Mambo mazuri kati ya Tanzania,Afrika Kusini kuhusu elimu yashika kasi

NA MWANDISHI WETU

UTEKELEZAJI wa Hati ya Makubaliano ya ushirikiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini kwenye maeneo mbalimbali ya elimumsingi umeanza kwa kasi ambapo leo Julai 28, 2022 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ameshuhudia uwekaji saini wa rasimu ya Mpango Kazi wa Utekelezaji wa Makubaliano hayo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam mara baada ya kushuhudia tukio hilo, Waziri Mkenda amesema, hatua hiyo inatoa mwelekeo wa jinsi ya kushirikiana baina ya nchi hizo mbili kwenye elimu hususan ufundishaji wa lugha ya Kiswahili pamoja na mitaala.

Amesema lengo la uwekaji saini huo ni kila upande kati ya Tanzania na Afrika Kusini ujifunze kwa mwenzake kusaidia kuendeleza Kiswahili.
"Baada ya kusaini Hati ya Makubaliano Julai 7, 2022 tulikubaliana na Waziri mwenzangu anayeshughulika na Elimu nchini Afrika Kusini kwamba tusiwe na hati ya makubaliano tu halafu tukaiweka kabatini, bali timu zikutane kuweka mpango kazi wa utekelezaji," amesema Prof. Mkenda
Amesema, kikubwa kwenye makubaliano hayo sio kufundisha Kiswahili tu lakini kuweka msukumo katika kuendeleza Kiswahili katika Bara la Afrika.

Aliongeza kuwa, Tanzania ina wajibu mkubwa wa kukuza Kiswahili na kuhakikisha kinasambaa katika nchi zote Afrika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news