NA DIRAMAKINI
MBUNGE wa Jimbo la Monduli wilayani Monduli Mkoa wa Arusha, Fredrick Lowassa ametoa shilingi millioni 3.8 kwa ajili ya ukarabati wa paa la Soko Kuu la Monduli.

Awali akizungumza mmoja wa wafanyabiashara katika soko hilo ambaye hakutaka kutajwa majina yake amesema changamoto yao kubwa ni miundombinu ya soko hilo, pamoja na kuomba kuondolewa kwa soko moja kwani wamekuwa wakimwaga vitu kutokana na kuharibika, kwani masoko yamekuwa mengi maarufu kama magulio.
Josephat Mbilinyi ni mwenyekiti wa soko hilo amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo pamoja na ukosefu wa mikopo zile asilimia kutoka halmashauri kwenda kwa wajasiriamali.
Pia Mbunge Lowasa ametoa ahadi ya pikipiki 12 ambazo zitatolewa wiki ili ziweze kunufaisha kila kijiwe kilichopo Monduli Mjini.