Msigwa awauma sikio wanahabari kuhusu sheria

NA DIRAMAKINI

MKURUGENZI wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali,Gerson Msigwa amesema,wakati Serikali na wadau wakiwa wameonesha dhamira ya kushirikiana katika mchakato mzima wa kupitia upya Sheria ya Huduma za Habari Namba 12 ya mwaka 2016, kila mmoja ana wajibu wa kuzingatia sheria zilizopo sasa.

"Kwa sababu tumeanza kuona dalili kwa baadhi ya vyonbo vya habari kuanza kuvunja sheria, kuvunja taratibu, kukiuka maadili ya uandishi wa habari hiki kitu sio sawa. Na ningependa kutumia nafasi hii kuwaomba sana waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya habari tuzingatie weledi wetu, nchi yetu ina sheria, tuzingatie sheria zetu;
Msigwa ameyasema hayo leo Julai 13, 2022 kando ya mkutano wa wadau wa maendeleo uliofanyika New Africa Hotel (Four Points by Sheraton Dar es Salaam) ambapo umefunguliwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye.

"Wadau wameonesha nia ya kushirikiana na Serikali na waandishi wa habari na wadau wa habari mimi nininachoomba ndugu zangu waandishi wa habari,Serikali imeonesha dhamira ya kufanyia kazi maoni yetu, basi naomba tuendelee kuzingatia sheria ambayo ipo kwa sasa kwa sababu kwa mujibu wa utaratibu, sheria inapopitiwa haina maana kwamba sheria iliyopo imesimama kufanya kazi.

"Inaendelea kufanya kazi,tuoneshe dhamira ya kushiriki katika mchakato huu kwanza kwa kuzingatia sheria iliyopo kwa sasa, pili katika utendaji wetu wa kazi tuioneshe Serikali kwamba tuko tayari kufanya kazi kwa ushirikiano,"amesema Msigwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news