NA MWANDISHI WETU
MTUMISHI wa Shirika la Umeme (TANESCO) anayefahamika kwa jina la Yahaya Abdul, mkazi wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi amekutwa amefariki dunia katika nyumba ya kulala wageni alikoenda kujipumzisha na rafiki yake wa kike.
Kwa upande wake mhudumu wa nyumba ya kulala wageni ameeleza kuwa, marehemu alifika majira ya saa 7:00 mchana na mpenzi wake lakini ameshangazwa kuona pikipiki ya mtu huyo mpaka asubuhi ikiwa pale gesti.
Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi , Emmanuel Tinda, amekiri kupokelewa kwa mwili wa mtu ambaye jina lake halijafahamika na uchunguzi wa kitabibu ili kubaini kifo chake unaendelea.
Aidha, mwanamke huyo ambaye alikuwa naye gesti anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo.