Nafasi ya uongozi ndani ya CCM haina miliki, kila mmoja yupo huru kugombea-Kinana

NA SAID MWISHESHE

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulrahman Kinana amesema nafasi za uongozi ndani ya chama hicho haina miliki na kwamba kila mtu anayo nafasi ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi, hivyo wajitokeze kugombea.
Aidha awapongeza wanachama wa Chama hicho Mkoa wa Songwe kwa namna walivyofanikisha uchaguzi huku akitoa rai kwa wanawake na vijana kujitokeza kuomba nafasi za uongozi.

Kinana ameyasema hayo leo Julai 27,2022 wakati akizungumza na wanachama wa CCM Mkoa wa Songwe kwenye kikao cha ndani ambapo ametumia nafasi hiyo kuwapongeza wote ambao wamechaguliwa hadi sasa na waliokosa wawe na subira.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulrahman Kinana akizungumza na wanachama wa CCM Mkoa wa Songwe kwenye kikao cha ndani Julai 27,2022 akiwapongeza kwa namna walivyofanikisha uchaguzi huku akitoa rai kwa wanawake na vijana kujitokeza kuomba nafasi za uongozi,wakati huo huo akawaeleza kuwa nafasi za uongozi ndani ya Chama hicho haina miliki na kwamba kila mtu anayo nafasi ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi, hivyo wajitokeze kugombea.(PICHA NA MICHUZI JR-SONGWE).

“Niwapongeze wanaogembea nafasi za Kata na naamini wanachama watachagua viongozi bora na wanaokubalika, uzuri wa Chama hiki kina demokrasia na kila baada ya kipindi fulani uongozi naisha.

“Uongozi hauna hati miliki, ukikalia kwenye kiti usikalie kama umepiga msumali, kaa ukijua baada ya miaka mitano nafasi iko wazi , kila baada ya miaka mitano unagombea na ukiona kuna mtu anagombea nafasi yako sio dhambi na hata wewe kama ni katibu au mjumbe haukuzaliwa nao.
“Kuna mtu ulimtoa, sasa kuna dhambi gani nikikutoa, na nakutoa kwa hoja kwa kukubalika, nakutoa kwa kukubalika na wananchi, hivyo tushindane na nikikutoa nipe mkono tuagane.Tusitumie nafasi zetu kuzuia wengine,”amesema Kinana.

Aidha amesema lazima wakubali kila mtu anafasi sawa na mwenzake, hivyo aliyekuwa kwenye nafasi ajiandae halafu watakutana na wajumbe wakati wa kupiga kura.

“Nawajumbe wenyewe wanamwambia kila mtu usiwe na wasi wasi, siku hizi wajumbe wanaogopwa.Ninachojaribu kusema sisi lazima tuoneshe demokrasia ndani ya Chama chetu lakini mniruhusu niwaombe wanawake wengi kugombea nafasi

“Kwa mujibu wa takwimu za Mkoa wa Songwe kuna watu 650,000 na kati yao wanawake ni asilimia 58 ni wanaume ni asilimia 42 , hivyo lazima wanawake nao wawe wengi kwenye nafasi za uongozi. Wanawake wanaaminika kuliko wanaume.
wanachama wa CCM Mkoa wa Songwe wakiwa kwenye kikao cha ndani Julai 27,2022 wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulrahman Kinana alipokuwa akizungumza nao kwenye kikao hicho cha ndani

“Wanawake wanajua kujituma kuliko wanaume, wanawake ni mahodari kuliko mimi na wenzangu, wanawake wanajua kutunza fedha kuliko sisi, wanaume hata kama hamkubali lazima mkubali hata kweli mchungu,”amesema.

Kinana amesema ni vema akina mama na vijana wakapewa nafasi kwa wingi , hivyo wajitokeze kuomba nafasi, nchi yetu inaongozwa kwa kupokezana nafasi, na vijana ni vema wakawa wengi kwenye uongozi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news