NA DIRAMAKINI
NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu ameshiriki Kikao cha Kamati ya Maendeleo Endelevu ambayo ni moja ya Kamati Sita za Bunge la Kimataifa linaloshughulikia masuala ya Uvumilivu na Amani (International Parliament for Peace and Tolerance).
Vikao vya Kamati hizo vimefanyika Julai 13, 2022 katika Bunge la Morocco vikitangulia Mkutano wa 10 wa Bunge hilo ambao utafunguliwa rasmi leo Julai 14, 2022 na vikao vyake kumalizika Julai 16, 2022.
Kauli mbiu ya Mkutano huo ni ‘Securing food: a key prerequisite for Global Peace and Tolerance’...(Kupata chakula: Hitaji kuu la Amani na Ustahimilivu Ulimwenguni).
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu ameshiriki Kikao cha Kamati ya Maendeleo Endelevu ambayo ni moja ya Kamati Sita za Bunge la Kimataifa linaloshughulikia masuala ya Uvumilivu na Amani (International Parliament for Peace and Tolerance).(PICHA NA BUNGE).