NA MWANDISHI WETU
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) Julai 20, 2022 amefanya ziara ya kushtukiza katika eneo la Shule ya Msingi Sagani lililopandwa miti kwenye Maadhimisho ya Siku ya Upandaji Miti Kitaifa yaliyofanyika Machi 21, 2022 Wilayani Magu Mkoani Mwanza.

Mhe. Masanja amemuagiza Mkuu wa Shule ya Msingi Sagani, Ruhumbika Kapesa, kuendelea kusimamia ukuaji wa miti hiyo ili ifikie lengo lililokusudiwa la kuifanya Wilaya ya Magu kuwa ya kijani.