NA MWANDISHI WETU
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene amepongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma kwa kutekeleza vizuri zoezi la anwani za makazi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe.George Simbachawene akikagua utekelezaji wa operesheni anwani makazi katika Kijiji cha Mpwanila Kata ya Luhundwa katika Jimbo la Kibakwe Halmashauri ya Mpwapwa.
“Uwekaji wa anwani za makazi unaenda sambamba na zoezi la sensa ili kujua katika ramani mahali mitaa, barabara zilipo. Mmefanya jambo zuri ambalo watu wengine wanapaswa kuja kujifunza alisema waziri;
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu sera Bunge na Uratibu (Mb), Mhe, George Simbachawene katika ziara aliyoifanya Kata ya Pwaga na na Luhundwa alipotembelea na kufanya Mikutano.
“Haya ni maelekezo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ambaye aliagiza operesheni ya postikodi ili watanzania wajulikane wanakaa wapi; jambo la kuweka mitaa, lakini pia barabara na namba kwenye nyumba katika Halmashauri Wilaya ya Mpwapwa na jimbo la Kibakwe limefanyika kwa mazingira makubwa;
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe.George Simbachawene akikagua utekelezaji wa Operesheni anwani Makazi katika Kijiji cha Ikuyu kata ya Luhundwa katika jimbo la kibakwe halmashauri ya Mpwapwa.