NMB kurahisisha udhibiti makusanyo ya mapato Sekta ya Utalii Zanzibar

NA DIRAMAKINI

BENKI ya NMB katika kuhakikisha Sekta ya utalii visiwani Zanzibar inaimarika, imekabidhi Mashine za Malipo (POS) 50 pamoja na Lipa Mkononi (QR) kusaidia kudhibiti na kukuza ukusanyaji mapato katika Sekta ya Utalii visiwani Zanzibar.
Mkuu wa Biashara ya Kadi Benki ya NMB,Philbert Casmir (katikati), akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar,Dkt.Amina Ameir Issa, mfano wa mashine ya kupokea malipo kwa ajili ya wizara hiyo. NMB imekabidhi mashine 50 ambazo zitasaidia kuimarisha na kukuza ukusanyaji wa mapato kwenye Sekta ya Utalii. Kutoka kushoto ni Meneja Mwandamizi Biashara ya Kadi NMB,David Ngusa na Meneja Biashara NMB Zanzibar,Naima Said Shame.

Akizungumza katika hafla ya makabidhino, Mkuu wa Idara ya Biashara za Kadi NMB, Philbert Casmir alisema, “huu ni utekelezaji wa makubaliano tuliofanya miezi sita iliyopita kati ya Benki ya NMB pamoja na Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar. Tulisaini makubaliano ya kuimarisha uchumi wa bluu kwa kutoa elimu na kuhamasisha watu kutembelea vivutio vya kitalii,"alisema.
Mkuu wa Biashara ya Kadi Benki ya NMB, Philbert Casmir (katikati), akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Dk. Amina Ameir Issa, mfumo wa malipo wa Lipa Mkononi (QR) kwa ajili ya wizara hiyo. Kushoto ni Meneja Biashara NMB Zanzibar - Naima Said Shame.

Akipokea mashine hizo pomoja na Lipa Mkononi (QR) Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Dkt.Amina Ameir Issa alisema kuwa Benki ya NMB imerahisisha malipo, sasa unamaliza malipo kidijitali kwani ukienda kwenye vituo vya utalii huna haja ya kubeba fedha taslimu. 

"Uwe Mtanzania au mgeni, unalipia kwa mashine hizi kwa kutumia kadi yako ya benki, ambayo inapokea mifumo ya MasterCard, VISA na UnionPay au simu za mkononi kutumia mfumo wa Ku-scan au Lipa Namba kufanya malipo,"amesema.

Aidha, alieleza kuwa sasa Serikali itaweza kujua kiwango cha fedha kinachoingia kwa siku, wiki, mwezi au mwaka hivyo kuwawezesha kufikia malengo ya mwaka huu wa fedha ya kukusanya Sh. Bilioni Moja katika sekta ya utalii. Maeneo yatakayotumia mfumo huu ni pamoja na Mvuleni, Kizimkazi, Mapango ya watumwa Manga Pwani, Bi Khole, Mtoni, Rasi ya Kibweni na Maruhubi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news