NA MATHIAS CANAL
WAKALA wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) imetakiwa kujitathmini kutokana na kadhia ya kushindwa kusimamia mradi wa maji wilayani Rombo Mkoa wa Kilimanjaro.
Mbunge wa Jimbo la Rombo ambaye pia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,Mhe. Prf Adolf Mkenda ametoa kauli hiyo Julai 26, 2022 wakati akiwa katika muendelezo wa ziara jimboni humo ambapo amekagua ujenzi wa mradi wa maji wa shilingi bilioni 2.9.
Prof.Mkenda amekagua mradi huo ambao mkandarasi alisaini kuanza kazi mwanzoni mwa mwaka huu 2022, lakini mpaka sasa hakuna kazi iliyokwisha kufanyika zaidi ya kuwekwa mchanga na kokoto zisizozidi hata gari moja.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgnABIodUlJF08ZTKGhqd3MYTUGA878cLxWsbKeiEzKGlhAvrXlxTUyCmcjLkhaBLBuZSHh6RJ71H2SoRdZAZmiste9KtIyBur1iq1gBZfIaEGmRy5RbI8qTejJ196oemown1fcxjNtwV4c4PrlJGW5iWDCuJ4AitXTOZN1OSVQOdBSfi4Ljb3g9IMxfg/s16000/IMG-20220728-WA0022.jpg)
"Tatizo namba moja, mbili, na tatu Rombo ni maji sasa mtu anayechezea mradi wa maji sielewi ana madhumuni gani na anataka wananchi wa Rombo wawe na taswira gani kwa serikali, wanamhujumu Waziri wa Maji Mhe.Juma Aweso ambaye ni mchapakazi na kwa hili nitamualika aje aone changamoto hii,"amesema Prof.Mkenda.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj9idoLakeL-0BEH6PIYzobiOebfkmWHfpxaYzet0wAo29EfsnppzeMrgqfNwY6qBg66jMX8sUwZYB7-8rTym9IWnueKs3k0puhCxED9cXXRzXS0tYyczf7Gun8aF0QXpLf2n3bvEjRuniJXDEquMfv8R2ZyytriYA4cuKP6rwAbQh-9pqVR5b-xpZBlQ/s16000/IMG-20220728-WA0035.jpg)
"Kwa kuwa sehemu hii ni ngumu kufika sio rahisi kwa viongozi kufika na kuona maendeleo ya mradi huo inakuwa rahisi kuficha mapungufu haya kwa hiyo RUWASA inabidi ijiangalie upya kwa kuwa ndio msimamizi wa mradi huu,"amesisitiza Prof. Mkenda.