PURA yadhamiria makubwa kwa wawekezaji

NA DIRAMAKINI

MAMLAKA ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imesema imedhamiria kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi hasa wa ndani,ambapo imeanzisha Kanzi Data ambayo imelenga kusaidia wataalam mbalimbali wa masuala ya mafuta na gesi kupata ajira kwa urahisi zaidi.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Ushiriki wa Wazawa na Ushirikishwaji wa Wadau PURA, Charles Nyangi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 46 yanayoendelea katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.

Amesema,PURA kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) wameanzisha Kanzi Data (CQS) hiyo ambayo itawezesha kampuni na mtu mmoja mmoja kujisajili na kushiriki mchakato wa utafutaji na uchimbaji na mafuta nchini.

"Kupitia Kanzi Data hii itawezesha kila mtu anayetaka kushiriki katika eneo hilo la utafutaji na uchimbaji wa gesi kupata taarifa mbalimbali zinazowekwa na PURA kila kitu ambacho kitahitajika kwa mwekezaji kinakuwepo kwenye CQS hiyo,"amesema.

Amebainisha kuwa, Kanzi Data hiyo imeanza kutumika tangu mwezi Mei, mwaka huu,ambapo wameanza kuandikisha kupitia website yetu na fomu maalum ambazo wanajaza.

Mkuu huyo wa kitengo ameongeza kuwa, katika maonesho hayo wamekuwa wakitoa elimu na uhamasishaji wa ushiriki wa wazawa katika shughuli za mkondo wa juu wa Petroli.

"Kupitia Maonesho haya ya 46 tumekuwa tukitoa elimu kuhusu fursa zinazopatina nchini katika eneo la gesi na mafuta, PURA tutaendelea kutoa elimu ya umuhimu wa wazawa kushiriki katika kazi za uchimbaji, ununuzi, ukaratabati na nyingine ambazo zinafanyika katika eneo hilo,"amesema. 

Aidha, ametoa wito kwa Watanzania wote kuendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali ambazo zitahitaji ushiriki wao.

Akizungumzia kuhusu ushiriki wa watanzania katika Shughuli za mkondo wa juu wa Petroli amesema, kwa miaka ya karibuni baada ya kuanzishwa kwa Sheria umeongezeka kwa kiasi kikubwa.

Amesema zaidi ya asilimia 90 ya waajiriwa katika kampuni za gesi asilia ni watanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news