Rais Dkt.Mwinyi:Serikali itatoa ufadhili nafasi 30 za vyuo kwa wanafunzi waliofanya vizuri

NA DIRAMAKINI 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa, Serikali itatoa ufadhili wa nafasi 30 za masomo ya vyuo vikuu kwa wanafunzi wa kidato cha sita waliofanya vizuri kwenye mitihani ya mwaka huu.
Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi ameyabainisha hayo baada ya kujumuika katika hafla maalumu aliyowaandalia wanafunzi waliofanya vizuri mitihani yao ya Taifa katika viwanja vya Ikulu ndogo Pagali kisiwani Pemba.

Hafla hiyo ambayo imefanyika Julai 29,2022 imehusisha chakula cha pamoja na utoaji zawadi maalumu kwa wanafunzi hao.
"Nimejumuika na kuwapongeza wanafunzi waliofaulu mitihani ya kidato cha nne na cha sita Ikulu Pagali, Pemba. Serikali itatoa ufadhili wa nafasi 30 za masomo ya vyuo vikuu kwa wanafunzi wa kidato cha sita waliofanya vizuri kwenye mitihani ya mwaka huu,"ameeleza Rais Dkt.Mwinyi.

Juhudi hizo zinaenda sambamba na mipango mikakati ya Serikali ya Awamu ya Nane chini ya Mheshimiwa Rais Dkt.Hussein Ali Mwinyi ambayo licha ya kuendelea kuwekeza katika ubora wa elimu na upatikanaji wake Zanzibar pia inajenga na kuimarisha miundombinu ya kisasa ili wanafunzi waweze kusomea katika mazingira mazuri.

Katika hafla hiyo, mfanyabiashara maarufu, Bw. Said Bopar alitoa zawadi za kompyuta mpakato kwa wanafunzi waliopata alama ya daraja la kwanza kwenye mitihani waliofanya ya kidato cha nne na cha sita.

Baadhi ya wanafunzi wa skuli za sekondari Pemba waliofaulu vizuri mitihani yao ya Taifa wakipata chakula maalumu kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi katika viwanja vya Ikulu ndogo Pagali Pemba leo Julai 29,2022, wakati wa hafla ya kuwapongeza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news