NA DIRAMAKINI
SIKU tatu baada ya Dkt.Raphael Chegeni kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, uteuzi wake umetenguliwa.

Rais Samia alimteua Dkt.Raphael Chegeni kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Julai 28, 2022 kuchukua nafasi ya Ally Hapi.
Katika
taarifa ya Ikulu imesema, mkuu huyo wa nchi amemtengua uteuzi wa
Dkt.Chegeni huku nafasi hiyo ikichukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la
Magereza Tanzania, Meja Jenerali Suleiman Mzee.

"Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Meja
Jenerali Suleiman Mzee kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara na kutengua uteuzi wa
Dkt.Raphael Masunga Chegeni,” imesema taarifa hiyo.