Rais Samia ni kiongozi mchapakazi asiye na majivuno-Kinana

NA MWANDISHI WETU

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema licha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuzungumza polepole, lakini vitendo vyake katika utekelezaji wa sera za maendeleo zimekuwa motomoto.Pia, Serikali yake kwa muda mfupi imeaminika na kuheshimika kikanda na kimataifa.Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana alipokuwa katika Manispaa ya Jiji la Mbeya.

Kinana amesema, Rais Samia amekuwa kiongozi wa mfano ambaye kwa kipindi kifupi cha mwaka mmoja amekubalika katika medani za kidiplomasia huku akiaminiwa na taasisi za kimataifa.

Akizungumzia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020-2025, alisema serikali yake imekuwa ikitekeleza wajibu hatua kwa hatua na kuimarika kwa huduma za jamii.

"Rais Samia kiongozi mchapakazi asiye na majivuno. Kila uendapo utakutana na maendeleo ambayo hayakutegemewa yatokee haraka. Anazungumza polepole lakini vitendo ni vizito," alisema Kinana.

Aidha, Makamu huyo Mwenyekiti alisema, uongozi bora hupimwa kwa kutoa matokeo chanya ambayo kwa bahati nzuri kila sekta imepatiwa fedha za kufanikisha miradi ya maendeleo.

"Kila eneo limeguswa katika maendeleo. Sekta za maji,afya,elimu zimepatiwa fedha kusukuma mbele kwa muktadha wa kupunguza kero na kumaliza changamoto sugu,"amesema Kinana.

Hata hivyo kiongozi huyo aliwataka wanawake wengi zaidi kujitokeza katika kuwania nafasi za uongozi ili kukamilisha ndoto zao na kusema wanawake ni waaminifu na wasimamizi makini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news