Reli ya Kisasa (SGR) Dar-Moro mambo safi

NA DIRAMAKINI

LENGO la reli ya kisasa ni kuongeza ufanisi katika sekta ya usafirishaji nchini ususani sekta ya reli ambapo yafuatayo yatarahisishwa.
Mosi,ongezeko la usafirishaji wa mizigo ambapo reli itabeba mzigo wa mpaka tani 10,000 kwa mkupuo sawa na uwezo wa malori 500 ya mizigo.

Pili uokoaji wa muda kwa usafiri wa abiria na mizigo ambapo itasaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Tatu, ongezeko la ajira kwa wazawa katika sekta na fani mbalimbali. Nne, uboreshaji wa huduma za kijamii ikihusisha ujenzi wa shule, vituo vya afya na ujenzi wa barabara katika maeneo yanayopitiwa na mradi.

Tano, kuchochea maendeleo katika secta ya kilimo, biashara, madini na viwanda hususani katika maeneo ambapo reli hiyo inapita pamoja na kwa nchi jirani hasa Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya na DRC.

Sita, faida za kiuchumi kwenye sekta ya usafirishaji hasa kupunguza gharama za mara kwa mara za matengenezo ya barabara.

>Ujenzi wa reli ya kisasa kwa nchi yetu wenye mtandao wa kilomita 1,219 za njia kuu, upo katika awamu tano na ni kama ifuatavyo;

1:Awamu ya Kwanza ni Dar es Salaam-Morogoro (Km 300)

2:Awamu ya Pili ni Morogoro- Makutupora (Km 422)

3:Awamu ya Tatu ni Makutupora –Tabora (Km 294)

4:Awamu ya Nne ni Tabora-Isaka (Km 130)

5:Awamu ya Tano ni Isaka-Mwanza (Km 249)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news