NA FRESHA KINASA
MKURUGENZI wa Shirika la Hope for Girls and Women in Tanzania (HGWT), Rhobi Samwelly amepewa fursa ya kuzungumza kueleza kazi anazofanya mbele ya kusanyiko kubwa la waumini wa The American Church in Paris (ACP).

Miongoni mwa kazi ambazo Rhobi amekuwa akifanya kupitia shirika analoliongoza ni pamoja na mapambano ya vitendo vya ukatili wa kijinsia, kutetea usawa wa kijinsia pamoja na kutetea haki za binadamu.

Ambapo katika Mkoa wa Mara Shirika la Hope for Girls and Women in Tanzania (HGWT) lina vituo viwili vinavyotoa hifadhi kwa wasichana ambao hukimbia aina mbalimbali za ukatili kikiwemo Kituo cha Hope Mugumu Nyumba Salama kilichopo Mugumu Wilaya ya Serengeti na Kituo cha Nyumba Salama kilichopo Kiabakari Wilaya ya Butiama.