NA MWANDISHI WETU
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Prof. Godius Kahyarara amesema Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria kuiona Tanzania inakuwa lango la Uchumi wa Bara la Afrika kwa kuwa na Viwanda vikubwa ambavyo vitasaidia kupeleka Bidhaa kwenye Soko la Afrika kuongeza ajira na pato la Taifa.

Prof.Kahyarara ameyasema hayo Julai 5, 2022 alipokuwa akifungua Kongamano la Wawekezaji, Wauzaji na Wanunuaji lililofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam kama sehemu ya Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalianza tarehe 28 Juni hadi 13 Julai 2022

Aidha, amesema Serikali imetenga maenwo mbalimbali ya uwekezaji ikiwa ni ni pamoja na uwepo wa kongani za viwanda zinazotarajiwa kuwa na viwanda vya kuchakata mazao na kuzalisha bidhaa mbalimbali pamoja maeneo maalumu ya uzalishaji bidhaa kwa ajili ya mauzo ya nje hususani karibu na viwanja vya ndege.

Prof. Kahyarara pia ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutoa kipaumbele katika kukuza uchumi kwa kuchukua hatua mbalimbali za diplomasia ya uchumi ikiwemo filamu ya Royal Tour ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya kiuchumi.
Tags
Habari
Hali ya Uchumi
Kituo cha Uwekezaji Tanzania
Lango la Uchumi Afrika
Uchumi na Biashara
Uwekezaji
Wizara ya Uwekezaji na Biashara