Serikali imedhamiria kujenga na kukarabati skuli zote za zamani-Rais Dkt.Mwinyi

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameweka jiwe la msingi la skuli ya Sekondari Pujini na kueleza jinsi Serikali ilivyodhamiria kujenga skuli za ghorofa kama hizo ili kupunguza changamoto ya uhaba wa madarasa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizungumza baada ya kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Skuli ya Pujini Wilaya ya Chakechake Pemba wakati akiendelea na ziara yake katika Mkoa wa Kusini Pemba.(Picha na Ikulu).

Pia alieleza azma ya serikali ya kujenga na kuzifanyia ukarabati skuli zote za zamani ili ziweze kukidhi kusaidia katika kuondoa changamoto katika sekta hiyo ya elimu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mhandisi wa Kampuni ya Ujenzi ya Mwinyi Bulding Contractor, Alawi Abdalla Ahmed wakati akitoa maelezo ya kitaalum ya michoro ya ujenzi huo,kushoto kwa Rais ni Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Lela Mohammed Mussa na kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mhe. Mattar Zahro Masoud.(Picha na Ikulu).

Ameyasema hayo Julai 27, 2022 wakati akiwa katika mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo ya Mkoa wa Kusini Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Skuli ya Pujini inayojengwa kwa Fedha za Uviko-19.(Picha na Ikulu).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news