'Serikali itahakikisha inapata ufumbuzi changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu'

NA MWANDISHI WETU

NAIBU Waziri Mary Masanja (Mb) amesema kuwa Serikali itahakikisha inapata ufumbuzi wa changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu wanaovamia makazi ya watu hususan tembo.
Ameyasema hayo katika ziara ya kikazi alipotembelea Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) mjini Morogoro. Amesema kuwa, Serikali haifurahishwi na matukio ya wananchi kuuawa na tembo au kuliwa mazao yao.

"Serikali inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan haifurahii matukio ya tembo kuuwa watu kwa sababu uhai wa mtu hauwezi kurudishwa" Mhe. Masanja amesisitiza
Amesema moja ya mikakati ya kutatua changamoto hiyo ni kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mbinu za kukabiliana na tembo.

Ameongeza kuwa njia nyingine ya kutatua tatizo hilo ni kuwavisha tembo viongozi kola maalum ili kuwawezesha Askari Uhifadhi kujua mwelekeo wa kundi la tembo.

Pia, amesema Serikali inaendelea kutafuta mbinu za muda mrefu za kutatua changamoto hiyo.
Ziara hiyo ni mwendelezo wa ziara za kusikiliza changamoto za Taasisi na kuangalia utekelezaji wa majukumu yake iili kutafuta ufumbuzi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news