NA MWANDISHI WyEST
WITO umetolewa kwa viongozi wa taasisi na wadau wanaojishughulisha na utoaji wa Elimu Jumuishi, kuendelea kushirikiana na Serikali katika kujenga shule kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum.


"Serikali inatambua kuwa pamoja na kuwa na mfumo wa Elimu Jumuishi, bado kuna wanafunzi wenye mahitaji maalum ambao hawawezi kutumia mfumo huo kutokana na changamoto walizo nazo hivyo ni muhimu kuweka msukumo zaidi katika kuimarisha mifumo tofauti ya ufundishaji kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum kama vile shule maalum na vitengo," ameongeza Mhe. Kipanga.
Prof. Carolyne Nombo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu amewashukuru wazazi kwa kuwapeleka watoto wenye mahitaji maalum katika shule hiyo ili kupata Elimu.

Naye Dkt. Charles Msonde, Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI amesema Wizara yake imeleta walimu bora na mahiri kuja kufundisha shuleni hapo na ameahidi kuzifanyia kazi changamoto zote ambazo zipo katika shule hiyo ili kuendelea kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji shuleni hapo.
"Kazi ya walimu hawa inaonekana wazi ilivyo bora kwa jinsi wanavyowapa watoto hawa maarifa, ujuzi na stadi kwa nadharia na vitendo. Naamini baada ya miaka minne tutashuhudia makubwa sana kutoka kwa watoto hawa," amesema Dkt. Msonde

Akifafanua kuhusu shule hiyo, Dkt. Magreth Matonya, Mkurugenzi wa Elimu Maalum, Wizara ya Elimu amesema shule hiyo sio maalum bali ni jumuishi kwa kuwa inachukua wanafunzi wenye mahitaji maalum na wasio na mahitaji maalum.