NA OR-TAMISEMI
SERIKALI imemaliza kiu ya wananchi wanaotumia barabara ya Orthodox-Rwenkorongo-Chonyonyo kwa kutatua changamoto ya kutumia mitubwi kama njia ya usafiri kuvuka eneo la barabara lenye tingatinga umbali wa kilomIta 0.25 kwenda kupata huduma za kijamii.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa wakati akikagua barabara hiyo na kueleza kuwa Serikali ilepeleka kiasi cha milioni 417 kujenga baabara hiyo yenye umbali wa kilomita 16. 2 inayounganisha kata za Chonyonyo na Kamagambo wilayani Karagwe Mkoa Kagera.
“Tunamshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia milioni 417 ambazo zimefanya historia katika barabara hii ambayo wananchi walikuwa wakivuka kwa mitubwi, kwa sasa barabara imetengenezwa vizuri wanannchi wanapita bila shida,”amesema Bashungwa.
Bashungwa amepongeza Mkandarasi wa barabara hiyo Ruzubona Company Ltd kwa kazi nzuri ya ujenzi uliofikia asilimia 90 ambapo mkandarasi amekamilisha kazi za kuchonga barabara, kupanga mawe na kunyanyua eneo lenye maji, kujenga makalavati na kukata mlima.
Aidha, amemsisitiza mkandarasi kuendelea kufanya kazi yenye viwango kulingana na thamani ya gharama za ujenzi na akamsisitiza kuongeza umakini katika ujenzi wa eneo la daraja yanapopita maji pia katika mlima ambao unapaswa kupunzwa ukali na kujengewa kingo za maji ili sehemu hiyo ipitike kiurahisi.
Nae, Diwani wa Kata ya Kamagambo, Mhe.Mzakiru Mussa ameishukuru Serikali kwa kutatua kero ya muda mrefu ambayo iliyowalazimu wanannchi na wanafunzi kutumia mitumbwi kwenye msimu wa mvua kuvuka eneo hilo ambayo lilikuwa hatarishi kwa maisha yao.
Kwa mujibu wa mkataba, mkandarasi atachonga barabara urefu wa kilomita 16.2, kumwaga changarawe, kujaza mawe na udongo kwa ajili ya kuinua tuta eneo lenye maji, ujenzi wa mitaro pamoja ujenzi wa makaravati isa.