NA CHIKU MAKWAI
MAFUNZO ya ujuzi tepe (Soft Skills) yaliyokuwa yakitolewa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye ulemavu) kwa makundi maalumu ya vijana yamehitimishwa rasmi mjini Shinyanga.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Julius Tweneshe akizungumza wakati wa Kuhitimisha ya Mafunzo ya Ujuzi Tepe kwa Makundi Maalumu ya Vijana Wenye Ulemavu, wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (WAVIU) na Wamama Wadogo (Young Mothers) yanayohusu masuala ya Ujasiriamali, Usimamizi wa Biashara, Kujitambua, Afya ya Uzazi na Ujinsia yaliyofanyika katika Ukumbi wa Liga Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga yaliyofanyika kuanzia tarehe 28 Juni, 2022 hadi 30 Juni, 2022
Mafunzo hayo yaliyoanza kutolewa Juni 28, 2022 mwaka huu, yamehitimishwa leo Juni 30, ambayo yalikuwa yakihusisha makundi maalumu ya vijana wakiwamo wenye ulemavu, wa mama wadogo na ambao wanaishi na Virusi vya Ukimwi (VVU).
Akizungumza Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Julius Tweneshe amewataka wakurugenzi wa halmashauri za wilaya kuwapa ushirikiano vijana na kuwapatia mikopo na kuacha urasimu wa kuwanyima mikopo kwa kisingizio kwamba vijana hawarejeshi mikopo.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Julius Tweneshe akizungumza wakati wa Kuhitimisha ya Mafunzo ya Ujuzi Tepe kwa Makundi Maalumu ya Vijana Wenye Ulemavu, wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (WAVIU) na Wamama Wadogo (Young Mothers) yanayohusu masuala ya Ujasiriamali, Usimamizi wa Biashara, Kujitambua, Afya ya Uzazi na Ujinsia yaliyofanyika katika Ukumbi wa Liga Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga yaliyofanyika kuanzia tarehe 28 Juni, 2022 hadi 30 Juni, 2022
“Tunawajibu wa kuwalea na kuwajengea uwezo vijana waweze kukopa badala ya kuwakatisha tamaa. Hawa vijana tulio wapa mafinzo tuwape ushirikiano,”amesema.
Amesema Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) imetoa mafunzo ya ujuzi tepe kwa vijana wa makundi maalumu katika Manispaa ya Shinyanga, kupitia programu ya stadi za maisha kwa vijana walio nje ya mfumo wa shule ili kuwapatia Maarifa katika ya kujikwamua kichumi.
“Mafunzo ambayo tumetoa kwa vijana hawa makundi maalumu tunaimani yatakwenda kubadilisha mfumo wa maisha yao, sababu mbali na kuwapatia elimu hii, pia tuwaunga kwenye vikundi vya ujasiriamali ambavyo watakwenda kuanzisha shughuli mbalimbali na kuinuka kiuchumi,”amesema.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Julius Tweneshe akigawa cheti kwa mnufaika wa mafunzo ya Ujuzi Tepe wakati wa Kuhitimisha ya Mafunzo hayo kwa Makundi Maalumu ya Vijana Wenye Ulemavu, wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (WAVIU) na Wamama Wadogo (Young Mothers) yanayohusu masuala ya Ujasiriamali, Usimamizi wa Biashara, Kujitambua, Afya ya Uzazi na Ujinsia

Wanufaika wa mafunzo ya Ujuzi Tepe wakiwa ukumbini wakati wa Kuhitimisha ya Mafunzo hayo kwa Makundi Maalumu ya Vijana Wenye Ulemavu, wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (WAVIU) na Wamama Wadogo (Young Mothers) yanayohusu masuala ya Ujasiriamali, Usimamizi wa Biashara, Kujitambua, Afya ya Uzazi na Ujinsia
Wanufaika wa mafunzo ya Ujuzi Tepe wakiwa ukumbini wakati wa Kuhitimisha ya Mafunzo hayo kwa Makundi Maalumu ya Vijana Wenye Ulemavu, wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (WAVIU) na Wamama Wadogo (Young Mothers) yanayohusu masuala ya Ujasiriamali, Usimamizi wa Biashara, Kujitambua, Afya ya Uzazi na Ujinsia.
Aidha, amesema Serikali inatoa fursa mbalimbali za mikopo kwa vijana ikiwemo mfuko wa maendeleo ya vijana uliopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) ambapo Vijana wanaweza kuitumia kujikwamua kiuchumi.
Ameongeza kuwa mfuko huo wa maendeleo ya vijana kwa sasa wameuboresha ambao unatoa mkopo kuanzia kijana mmoja, na marejesho yake ni kuanzia miaka mitatu huku Riba yake ikipunguzwa kutoa asilimia 10 hadi Tano, Riba ambazo zimebaki kwa ajili ya ufuatiliaji na usimamizi wa mfuko.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga John Tesha, amewaasa vijana hao kupitia vikundi vyao vya ujasiriamali ambavyo wameviunda, wakamilishe taratibu zote na kisha wafike Halmashauri kwa ajili ya kuomba mkopo hiyo.
Pia, ametoa wito kwa vijana hao kupitia vikundi vyao vya ujasiriamali wakae na kufikiri na kuibua miradi yenye tija, ambayo itakuwa endelevu na kuwainua kiuchumi.
Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Idara ya Maendeleo ya Vijana Godfrey Massawe akizungumza wakati wa Kuhitimisha ya Mafunzo ya Ujuzi Tepe kwa Makundi Maalumu ya Vijana Wenye Ulemavu, wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (WAVIU) na Wamama Wadogo (Young Mothers)
Mwakilishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Godfrey Kajia akizungumza wakati wa Kuhitimisha ya Mafunzo ya Ujuzi Tepe kwa Makundi Maalumu ya Vijana Wenye Ulemavu, wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (WAVIU) na Wamama Wadogo (Young Mothers).
Kwa upande wao baadhi ya wanufaika wa mafunzo hayo akiwamo Rubeni Simoni na Masanja Wiliamu, kwa nyakati tofauti wamesema mafunzo hayo yamewasaidia kupata ujuzi na maarifa, ambayo watakwenda kuyatumia kujikwamua kimaisha kupitia fursa za mikopo zilizopo kwa vijana.