SIMBA SC SASA NI YA MOTO

NA DIRAMAKINI

WAKATI Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao 2022/23 ikitarajiwa kuanza Agosti 17,2022 na kumalizika Mei 27,2023 huku mchezo wa ngao ya Jamii ukitarajiwa kuchezwa Agosti 13,2022,Simba SC inakwenda kujiimarisha.

Kikosi kamili cha klabu hiyo kinatarajiwa kuondoka keshokutwa nchini kwenda kuweka kambi Misri kujiandaa na msimu huo.

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema, kikosi kitaondoka na wachezaji wote waliosajiliwa, kasoro wale watakaokuwa kwenye timu zao za taifa.

"Timu yetu itaondoka tarehe 14 mwezi huu kwenda kwenye mji wa Ismailia nchini Misri na itarudi Agosti 5. Tutaondoka na wachezaji wote isipokuwa wale ambao watakuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa. Tukirejea itakuwa ni Simba Day," amesema.
Wakati huo huo,Simba imemtambulisha kocha wake mpya, Zoran Manojilovic (Maji) ambaye amesaini mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongezewa mmoja akifanya vizuri. 

Simba SC wataondoka nchini ikiwa wanataka kufahamu pale walipoteleza hadi msimu ulioisha wa Ligi Kuu ya NBC kuambulia nafasi ya pili huku watani zao Yanga SC wakitwaa ubingwa. 

Aidha, mashabiki wa klabu hiyo yenye maskani yake jijini Dar es Salaam wanatarajia msimu ujao kuona mabadiliko makubwa ili shauku yao ya kutwaa mataji iweze kutimia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news