NA DIRAMAKINI
KLABU ya Simba imemtambulisha Mtunisia, Sbai Karim kuwa Kocha wa Viungo pamoja na Kocha Msaidizi sambamba na mzawa, Suleiman Matola.
Sbai na Matola watakuwa na jukumu la kumsaidia Kocha Mkuu, Zoran Maki kwenye kutimiza majukumu yake ipasavyo.
Aidha, inaelezwa kuwa, Sbai na Kocha Zoran wanafahamiana vizuri kwani wamefanya kazi pamoja katika Timu za Wydad Casablanca (Morocco), CR Belouzdad (Algeria) Al Hilal (Sudan) na Al Tai (Saudi Arabia) akiwa msaidizi wake.
Pia Sbai anatajwa kuwa ni kocha msomi mwenye leseni ya Daraja A ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).
Sbai ameifundisha Klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco kuanzia 2017 mpaka 2020 na kufanikiwa kuchukua mataji makubwa ya Afrika.
Msimu wa 2018/19 alicheza mchezo wa CAF Super Cup lakini timu yake ya Wydad ilipoteza mechi ambapo msimu wa 2020/2021 alikuwa akiitumikia klabu ya Al Hilal ya Sudan.