STAMICO watwaa tuzo mshindi wa jumla Sabasaba kwa ubunifu makini

NA DIRAMAKINI

SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limeibuka kidedea kwa kuwa mshindi wa jumla kwenye kipengele cha ubunifu makini (Overall Winner - Booth Creativity) katika maonesho ya 46 ya Sabasaba yaliyofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akimkabidhi tuzo kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse baada ya shirika hilo kuibuka mshindi wa jumla kwenye kipengele cha ubunifu makini (Overall Winner - Booth Creativity) katika maonesho ya 46 ya Sabasaba yaliyofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai 2022.

Tuzo hiyo ya STAMICO imetolewa tarehe 13 Julai 2022 na Mgeni rasmi Mhe. Dkt.Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa kufunga maonyesho hayo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akimuangalia Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse mara baada ya kumkabidhi tuzo ya ushindi kwa kwa shirika hilo baada ya kuibuka mshindi wa jumla kwenye kipengele cha ubunifu makini (Overall Winner - Booth Creativity) katika maonesho ya 46 ya Sabasaba yaliyofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai 2022.

Akipokea tuzo hiyo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse alisema, tunajivunia kupata tuzo hii ya jumla kutokana na ubunifu makini wa bidhaa bora ya mkaa mbadala wa kupikia (Rafiki Briquettes) unaotokana na Makaa ya Mawe. Mkaa huu ni njia madhubuti ya kuepusha ukataji wa miti hovyo kwa ajili ya nishati.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akisalimiana na mabalozi wa STAMICO baada ya kabidhi tuzo kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse baada ya shirika hilo kuibuka mshindi wa jumla kwenye kipengele cha ubunifu makini (Overall Winner - Booth Creativity) katika maonesho ya 46 ya Sabasaba yaliyofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai 2022 kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse na mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugezi ya STAMICO Meja Jenerali ( Mstaafu) Michael Isamuhyo.

Mkaa wa Rafiki Briquettes unaozalishwa na STAMICO ni Rafiki kwa mazingira, Rafiki kwa matumizi na Rafiki kwa bei. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugezi ya STAMICO Meja Jenerali ( Mstaafu) Michael Isamuhyo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse, Afisa Habari wa STAMICO, Bibiana Ndumbaro na mabalozi wa STAMICO wakielekea kwenye banda lao mara baada ya kupokea tuzo hiyo.  

Pamoja na tuzo ya ubunifu, STAMICO vilevile walipewa cheti cha ubora wa mpangilio wa bidhaa (Certificate of high display standard). 

Huu ni ushindi mara pili mfululizo kwa kipindi cha miaka miwili, mwaka jana 2021 kwenye maonesho ya 45 ya Sabasaba STAMICO iliibuka mshidi wa kwanza wa jumla.
Mabalozi wakiwa na tuzo huku wakiwa wameshika mkaa mbadala. 

Tukio hili limehudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugezi ya STAMICO Meja Jenerali ( Mstaafu) Michael Isamuhyo, pamoja na viongozi na wafanyakazi wa Shirika la Madini la Taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news