Tanzania, Algeria kufungua maeneo mapya ya ushirikiano

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) akipokea barua kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje ya Algeria iliyowasilishwa na Balozi wa Algeria nchini, Mhe.Ahmed DJELAL Julai  6,2022 jijini Dar es Salaam.
Mhe. Balozi Ahmed DJELAL akifafanua jambo kwa Mhe. Waziri Mulamula.
Mhe. Waziri Mulamula akizungumza na Mhe. Balozi Ahmed DJELAL, katika mazungumzo yao viongozi hao wamejadili juu ya kuimarisha ushirikiano baina ya Serikali zao hususan katika sekta za afya, nishati, elimu,miundombinu, usimamizi wa majanga, zimamoto na uokoaji.
Pia wamekubaliana kuanzishwa kwa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Algeria ili maeneo hayo ya ushirikiano yasimamiwe kwa tija ya mataifa yao.
Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini, Algeria, Mhe. Maj. Gen. Jacob Kingu akitoa ufafanuzi wakati wa mazungumzo hayo, kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga .
Mhe. Waziri Mulamula akiagana na Balozi Ahmed DJELAL baada ya mazungumzo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news