NA GODFREY NNKO
LEO Euro ya Ulaya (EUR) inanunuliwa kwa shilingi 2300.53 na kuuzwa kwa shilingi 2324.23 huku Dola ya Marekani (USD) inanunuliwa kwa shilingi 2292.96 na kuuzwa kwa shilingi 2315.89.
Hayo ni kwa mujibu wa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Julai 13, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Aidha,Paundi ya Uingereza (GBP) inanunuliwa kwa shilingi 2713.49 na kuuzwa kwa shilingi 2741.55 huku Rupia ya Pakistan (PKR) ikinunuliwa kwa shilingi 10.53 na kuuzwa kwa shilingi 11.13.
Franka ya Burundi (BIF) inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21 huku Dirham ya Umoja wa Falme za Kiarabu (AED) ikinunuliwa kwa shilingi 624.29 na kuuzwa kwa shilingi 630.48.
Yuan ya China (CNY) inanunuliwa kwa shilingi 341.01 na kuuzwa kwa shilingi 344.32 huku Yen ya Japan (JPY) ikinunuliwa kwa shilingi 16.77 na kuuzwa kwa shilingi 16.93.
Kwa upande wa Randi ya Afrika Kusini (ZAR) inanunuliwa kwa shilingi 134.52 na kuuzwa kwa shilingi 135.83 huku shilingi ya Kenya (KES) ikinunuliwa kwa shilingi 19.41 na kuuzwa kwa shilingi 19.58.
Franka ya Rwanda (RWF) inanunuliwa kwa shilingi 2.22 na kuuzwa kwa shilingi 2.28 huku shilingi ya Uganda (UGX) ikinunuliwa kwa shilingi 0.58 na kuuzwa kwa shilingi 0.61.
Tags
Bank of Tanzania Exchange Rates
Benki Kuu ya Tanzania
Fedha na Uchumi
Fedha za Kigeni
Indicative Exchange Rates from Bank of Tanzania