NA GODFREY NNKO
LEO dola ya Zimbabwe (ZWD) inanunuliwa kwae shilingi 0.43 na kuuzwa kwa shilingi 0.44 huku Euro ya Ulaya (EUR) inanunuliwa kwa shilingi 2358.77 na kuuzwa kwa shilingi 2383.28.
Aidha,Paundi ya Uingereza (GBP) inanunuliwa kwa shilingi 2748.11 na kuuzwa kwa shilingi 2776.52 huku Dinar ya Algeria (DZD) ikinunuliwa kwa shilingi 16.17 na kuuzwa kwa shilingi 16.19.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Julai 6, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Dirham ya Umoja wa Falme za Kiarabu (AED) inanunuliwa kwa shilingi 624.32 na kuuzwa kwa shilingi 630.43 huku Schilling ya Australia (ATS) ikinunuliwa kwa shilingi 147.14 na kuuzwa kwa shilingi 148.44.
Krona ya Sweden (SEK) inanunuliwa kwa shilingi 218.45 na kuuzwa kwa shilingi 220.57 huku Randi ya Afrika Kusini (ZAR) ikinunuliwa kwa shilingi 139.69 na kuuzwa kwa shilingi 141.04.
Shilingi ya Uganda (UGX) inanunuliwa kwa shilingi 0.59 na kuuzwa kwa shilingi 0.62 huku Franka ya Burundi (BIF) ikinunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21.
Kwacha ya Malawi (MWK) inanunuliwa kwa shilingi 2.08 na kuuzwa kwa shilingi 2.21 huku Rupia ya Pakistan (PKR) ikinunuliwa kwa shilingi 10.57 na kuuzwa kwa shilingi 11.21.
Rupia ya India (INR) inanunuliwa kwa shilingi 28.90 na kuuzwa kwa shilingi 29.17 huku Shilingi ya Kenya (KES) inanunuliwa kwa shilingi 19.45 na kuuzwa kwa shilingi 19.61.
Franka ya Rwanda (RWF) inanunuliwa kwa shilingi 2.20 na kuuzwa kwa shilingi 2.27 huku Kwacha ya Zambia (ZMK) ikinunuliwa kwa shilingi 137.16 na kuuzwa kwa shilingi 139.51.
Tags
Bank of Tanzania Exchange Rates
Benki Kuu ya Tanzania
Fedha na Uchumi
Fedha za Kigeni
Habari
Indicative Exchange Rates from Bank of Tanzania