Wafunguka kuhusu diplomasia ya uchumi na fursa za kiuchumi EAC

NA DIRAMAKINI

MJADALA wa dakika 150 ambao umeratibiwa na Watch Tanzania leo Julai 16, 2022 ukiangazia juu ya kukua kwa diplomasia ya uchumi na fursa za kiuchumi zinazopatikana ndani ya Afrika Mashariki (EAC) umetoa mwelekeo chanya huku washiriki wakishirikisha Watanzania fursa mbalimbali.

Kwa udhamini wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na Airtel Tanzania, washiriki wa mkutano huo maalum kupitia ZOOM wakiwemo wanadiplomasia na wadau wengine wameeleza kuwa; 
BALOZI WA TANZANIA NCHINI KENYA MHE.DKT.JOHN SIMBACHAWENE
"Tangu Rais Samia (Rais wa Jamhurin ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan) aingie madarakani ameshafanya ziara nchini Kenya mara mbili na kufanikiwa kusaini mikataba 12 katika maeneo ya afya, elimu, diplomasia, siasa, magereza,sheria na nishati, hii yote ni kukuza zaidi mashirikiano;"Kutokana na mashirikiano mazuri kati ya Tanzania na Kenya sasa mapato yameongezeka, mfano mzuri takwimu za hapa Tanzania kutoka TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) mwaka 2020 zinasema zimepanda kutoka bilioni 800 hadi trilioni 1.2 mwaka 2021,"amesema.

MOHAMMED DEWJI MFANYABIASHARA WA KIMATAIFA

"Tanzania kuna fursa nyingi sana, lakini leo tuongelee fursa ya pamba nchini, tunakila sababu ya kuwa wazalishaji wakubwa duniani wa pamba kwani mazingira yote mazuri tunayo kuanzia umeme, maji mpaka zao lenyewe kitu ambacho Kenya na Uganda hawana wingi wa zao hili;
"Takwimu zinasema matajiri wengi nchini Tanzania wanapatikana mikoani na sio mjini kwa vijana wengi wanavyodhani, fursa ya kilimo ni kubwa sana, mimi nilianza kulima katani ila mwisho wa mwaka huu kampuni yangu itakuwa ya kwanza duniani kwa uzalishaji wa katani,"amesema.

BALOZI MHE.DKT.JILLY MALEKO BALOZI WA TANZANIA NCHINI BURUNDI 

"Tanzania na Burundi kumekuwa na mahusiano mazuri sana tangu mwaka 1960 na viongozi mbalimbali kutoka Tanzania akiwemo Rais Samia wamekuwa na ziara za kitaifa nchini humu kwa ajili ya kuimarisha mahusiano haya.
"Mahusiano mazuri kati ya Tanzania na Burundi yalizidi kuimarika pale Burundi ilipojiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki tarehe 1/7/ 2007 na kuzidi kuboresha mazingira mazuri ya kibiashara na kiuchumi kwani asilimia 99 ya bidhaa zinazokuja Burundi zinapitia bandari ya Tanzania,"amesema. 

BALOZI WA TANZANIA NCHINI BURUNDI MHE.GERVAIS ABAYEHO 

"Burundi miaka ya nyuma kulikuwa na vita baina ya wao wenyewe kwa wenyewe na tunaishukuru sana nchi ya Tanzania kuweza kupokea wakimbuzi toka Burundi na kuwapatia hifadhi nchini.

"Miaka ya nyuma Burundi ilitawaliwa na vita hivyo sasa hivi ni wakati sahihi kabisa wa nchini mbalimbali duniani kwenda Burundi na kufanya uwekezaji katika maswala mbalimbali ya kiuchumi, nchi ya Burundi haina utofauti na msichana bikra,"amesema Balozi Abayeho. 

MHE.PROF GADIUS KAHYARARA KATIBU MKUU WIZARA YA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA 

"Umoja huu wa nchi za Afrika Mashariki umerahisishwa na itifaki ya soko la pamoja, ushuru wa pamoja, sheria za pamoja na uhuru wa wafanyabiashara kwenda kuwekeza nchi mbalimbali bila vikwazo vya aina yoyote; 
"Ndani ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia ndani ya uongozi wa nchi za Afrika Mashariki kumekuwa na mwingiliano mkubwa wa kiuchumi, fursa na biashara hii ni hatua kubwa sana kama nchi na inahitaji pongezi nyingi kwa Rais,"amesema. 

DANIEL CHONGOLO KATIBU MKUU CHAMA CHA MAPINDUZI

"Tukiangalia namna ambavyo Tanzania inakuwa kibiashara yaani kuuza na kununua bidhaa nje ya Tanzania inaonesha dhahiri kwamba Tanzania inakuwa kiuchumi na mahusiano yake baina na nchi zingine ni mazuri;
"Tukiendelea na wigo wa kuuza zaidi biadhaa zetu nje kama maparachichi, soya ambayo yanahitajika sana nchini China, mihogo, katani, pamba n.k hii itazidi kukuza reserves ya dola nchini na kufanya nchi kuimarika zaidi kiuchumi; 
MHE.DKT.ABDULLAH HASNUU MAKAME MBUNGE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI

"Kazi kubwa ya Mbunge wa Afrika Mashariki ni uwakilishaji wa wananchi kutoka nchi husika, kufuatilia utekelezaji wa mikataba ya Afrika Mashariki na kutunga sheria;
"Napenda sana kumpongeza Mhe.Rais Samia kwa ziara zake anazozifanya katika nchi mbalimbali ikiwemo nchi za Afrika Mashariki, kwani ziara hizi ndizo zinazozaa matunda ya mahusiano bora kati ya Tanzania na umoja wa nchi Afrika Mashariki,"amesema. 

BALOZI MHE.SAID JUMA MSHANA BALOZI WA TANZANIA NCHINI CONGO

"Nchi ya DRC inapakana na nchi tisa na idadi ya watu ni zaidi ya milioni 90 na ukubwa wa soko lake baada ya kujiunga na umoja wa Afrika Mashariki ni takribani milioni 300, eneo lake Tanzania inaingia mara mbili na nusu;
"DRC ina vyanzo 780 ya nishati vya kuzalisha umeme wenye Megawatts laki moja huku ni asilimia 2.5 tu ya vyanzo hivyo vimeendelezwa hivyo tuna mikakati ya kuendelea kuelezea wafanyabiashara walioko Tanzania kuja kufanya uwekezaji; 
MHANDISI LADISLAUS MATINDI MKURUGENZI MKUU SHIRIKA LA NDEGE LA TANZANIA (ATCL)

"Napenda kuwashukuru sana mabalozi wetu wa nchi mbalimbali kwani mchango wao kulifanya Shirika la Air Tanzania kukuwa ni mkubwa mfano ndege ya Air bus inayokwenda Kenya zamani ilikuwa inapandisha watu 10 tu ila leo ndege hiyo inajaza watu wote 120,"amesema. 
"Ifike hatua tuangalie Je? Baada ya kupata hizo fursa tunazotaka, tupo tayari kupambana na mataifa mengine ambayo yameshatangulia, mfano kama watalii wanakuja kupitia Air Tanzania, mawakala wa utalii Tanzania wapo tayari kupambana na mwakala wengine duniani; 
BALOZI MHE.DKT. AZIZ PONARY MLIMA BALOZI WA TANZANIA NCHINI UGANDA 

"Tumekuwa na majukwaa mawili ambayo tumekuwa tukishirikiana kati ya Tanzania na Uganda moja ni kushirikiana katika tume ya ushirikiano wa pamoja na pia umoja wa wafanyabiashara ulioanzishwa mwaka 2019 na mpaka sasa tumeshafanya majukwaa mawili tayari;
"Moja ya sababu kuwa, Tanzania hatupati watalii wengi toka Uganda ni kutokana na uchache wa safari za ndege, hivyo tukiweza kupambanua na kuongeza idadi ya safari hata mara nne kwa wiki itasaidia kuongeza idadi ya watalii kutoka Uganda; 

BALOZI MHE. SILIMA KOMBO HAJI BALOZI WA TANZANIA NCHINI SUDANI 

"Mwaka 1972 mpaka 2015 jumla ya mikataba tisa tuliweza kusaini kati ya Tanzania na Sudan kuimarisha mahusiano katika sekta ya Elimu, Utamaduni, Sayansi na Teknolojia, Biashara, Uchumi, utalii na n.k; 
"Tumekuwa tukiendelea kurekebisha sheria mbalimbali ambazo zitaendelea kuleta na kujenga mahusiano baina ya nchi za umoja wa Afrika Mashariki na Sudan yapokuwa Sudan haipo katika umoja huo, lakini upo katika nchi zilizopo ukanda wa Afrika Mashariki; 

MHE. JACQUELINE MKINDI MJUMBE WA BODI YA BARAZA LA BIASHARA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

"Nini kifanyike kwa Serikali kupitia fursa hizi zilizopo kwenye umoja wa Afrika Mashariki tuendelee kunufanika; 
1. Kuendelea kutengeneza mazingira rafiki ya uwekezaji kwa wawekezaji mbalimbali katika nchi hizi 

2. Kuendelea kuheshimu na kutekeleza makubaliano mbalimbali yaliyopitisha na kukubaliana 
3. Kila nchi husika kuendelea kuwekeza zaidi katika mifumo ya mawasiliano na ukusanyaji wa data 

4. Kujengeana uwezo wa kibiashara kwa serikali na umma 

5. Kuendelea kuaminiana na kushirikiana kufikia malengo 

"Kupitia mahusiano mazuri kati ya nchi ya Tanzania na Ubeligiji tumeweza kuuza mchele kutoka Mbeya kwenda Ubeligiji na wakulima Watanzania wameanza kunufaika,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news