Wamegewa siri ya kuliteka soko la Kimataifa

NA DIRAMAKINI

WITO umetolewa kwa wafanyabiashara nchini kuwa wabunifu na waadilifu katika kazi wanazozalisha ili waweze kuteka soko la Kimataifa.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt.Ashatu Kijaji katika maadhimisho ya miaka 15 ya utendaji kazi wa Kampuni ya GF Truck and Equipment Ltd yaliyofanyika ndani ya Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, kwenye maonesho ya 46 ya biashara Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya GF Truks,Imran Karmal akimkabidhi zawadi Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt.Ashatu Kijaji katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, kwenye maonesho ya 46 ya biashara Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.

Amesema, wateja wengi wamekuwa na malalamiko ya kupokea bidhaa tofauti na ile walioagiza hivyo anawataka wafanyabiashara wakiwemo wa mitandaoni kujenga imani kwa kutoa bidhaa halisi.

"GF Truck and Equipment Ltd wanafanya kazi nzuri sana, kwani magari wanayounganisha yana ubora na viwango vinavyokubalika na wateja wao wamekuwa wakipokea bidhaa zilizo bora,"alisema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa GF Truck and Equipment Ltd, Imran Karmal alisema hadi kufikia sasa wamefanikiwa kuunganisha gari la 600 na wamekuwa wakitoa ajira kwa vijana wa kitanzania.

"Malengo yetu ni kuendelea kuunganisha magari mengi zaidi kwa viwango na vigezo vya kimataifa, magari yetu yanaungwa na vijana wa kitanzania,"alisema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news