Watanzania wafanya kweli mchezo wa Kabaddi,kukata tiketi Kombe la Dunia

NA GODFREY NNKO

TANZANIA imejihakikishia kukata tiketi ya kushiriki mashindano ya Kombe la Dunia ya mchezo wa Kabaddi ambayo yatakafanyika mwezi Novemba, mwaka huu nchini India.
Sanjeevani kabaddi, ni mchezo maarufu wa kugusana Kusini mwa Bara la Asia ambao kwanza ulianzia India na sasa umeshika kasi katika kona mbalimbali za Dunia ikiwemo Tanzania.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mheshimiwa Mohamed Omary Mchengerwa ambaye ni Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo ikielezea kuhusu timu ya taifa ya mchezo wa Kabaddi wanaume na wanawake huko nchini Misri kwenye mashindano ya 3rd African Kabaddi Championship.

Amesema, mashindano hayo yalianza Julai 22 na yanatarajiwa kufikia tamati 28, 2022. "Timu zilizoshiriki ni wenyeji Misri, Tanzania, Kenya, Nigeria, Mauritania, Somalia, Djibouti,Cameroon.Ikiambatana na jumla ya watu 22, wachezaji 18 na viongozi watatu na kocha mmoja.

""Mchezo wa kwanza ulifanyika Julai 24, 2022 ambapo ilikuwa Tanzania 100 Vs Nigeria 7. Mchezo wa pili ulifanyika tarehe 24, Julai 2022 saa 12:30 jioni Tanzania 95 vs Kenya 5.

"Mchezo wa timu ya wanawake Tanzania Vs Mauritania haukuchezwa, timu pinzani ilisusa hivyo tukapata pointi za moja kwa moja kucheza fainali kwa timu ya kike baada ya kushinda mchezo mmoja.
"Kwa timu ya wanaume wamefanikiwa kushinda hatua ya makundi kuongoza group B timu ya wanaume imetinga nusu fainali baada ya kushinda nusu fainali tarehe 26 Julai, 2022. Tanzania 38 Vs Mauritania 4.

"Mchezo umekwisha tumefanikiwa kuingia fainali kwa timu zote mbili wanawake na wanaume fainali inachezwa hapo kesho Tanzania Vs Misri wanaume muda saa 12:5 jioni, Tanzania Vs Misri wanawake 11:00 asubuhi,"ameeleza Waziri.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news