Waziri Balozi Mulamula amuaga Balozi wa Pakistan nchini, ateta na Balozi wa Misri

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) amemuaga Balozi wa Pakistan hapa nchini Mhe. Mohammad Saleem anayemaliza kipindi chake cha kuhudumu.
Mazungumo baina Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula Balozi wa Pakistan anayemaliza kipindi chake cha kuhudumu nchini Mhe. Mohammad Saleem yakiendelea katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Katika tukio hilo ambalo limefanyika kwenye Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam Waziri Mulamula amemshukuru Balozi Saleem kwa utumishi uliotuka na kumpongeza kwa mafanikio makubwa aliyoyapata katika utendaji wake ambayo yataacha alama na kumbukumbu ya kudumu kwenye historia ya uhusiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Pakistan.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akimsikiliza Balozi wa Pakistan anayemaliza kipindi chake cha kuhudumu nchini Mhe. Mohammad Saleem alipokuwa akimuaga katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

“Wazara na Serikali kwa ujumla tunajivunia utendaji wako, katika kipindi chako ulichohudumu hapa nchini licha ya kudumisha na kukuza uhusiano baina yetu na Pakistan umefanya kazi nzuri sana ya kuibua fursa na mikakati mbalimbali ambayo imeleta manufaa kwa wananchi wetu, kama vile fursa za nafasi za masomo, kuendeleza shughuli za uvuvi nchini na kukuza biashara baina ya Tanzania na Pakistan,"amesema Waziri Mulamula.

Balozi Saleem kwa upande wake ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushirikiano mzuri iliompa katika kipindi chote alichokuwa nchini kuteleza majukumu yake. Aidha ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini usimamizi mahiri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri inayoendelea kuifanya ya kuleta maendeleo nchini.

Waziri Mulamula amemuhakikishi Balozi Saleem kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana kwa karibu na Pakistan kwa manufaa ya maslahi mapana ya pande zote mbili.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) na Balozi wa Misri nchini Tanzania Mhe. Mohamed Gaber wakiwa katika mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Wakati huo huo Waziri Mulamula amempokea na kufanya mazungumzo na Balozi wa Misri nchini Tanzania Mhe. Mohamed Gaber katika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam. Wawili hao wamejadili musaula mbalimbali yenye maslahi kwa pande zote mbili ikiwemo uwekezaji, biashara, elimu na mafunzo, ushirikiano katika sekta ya utamaduni na michezo na maendeleo ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali inayotekelezwa na Kampuni za Misri hapa nchini. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) na Balozi wa Misri nchini Tanzania Mhe. Mohamed Gaber wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Ubalozi na Wizara.

Aidha, wamekubaliana kuendelea kufuatilia utelezaji wa makubaliano na mikataba mbalimbali liyosainiwa wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan aliyoifanya nchini Misri mwezi Novemba 2021.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news