NA MWANDISHI WETU
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekutana na kufanya mazungumzo na Wenyeviti na Makatibu wa Vyama vya Wafanyakazi vilivyopo katika Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), ambapo wameongozwa na rais wa TUCTA, Tumaini Nyamhokya.




Katibu Mkuu TUCTA, Henry Mkunda, akieleza jambo wakati wa kikao cha Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Wenyeviti na Makatibu wa Vyama vya Wafanyakazi vilivyopo katika Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), jijini Dodoma tarehe 18 Julai, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Kikao hicho ni mwendelezo wa Serikali katika kuendelea kushirikiana na TUCTA katika kustawisha maslahi ya wafanyakazi husasni wa sekta Binafsi nchini.