Asilimia 99.9 ya Watanzania wamehesabiwa-NBS

NA DIRAMAKINI

OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema kuwa, asilimia 99.9 ya watanzania wamehesabiwa katika Sensa ya Watu na Makazi iliyoanza Agosti 23,mwaka huu.

Hayo yameelezwa leo Agosti 31,2022 na Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt.Albina Chuwa wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu Maendeleo ya Sensa ya Watu na Makazi,Sensa ya Majengo na Sensa ya Anwani za makazi hadi kufikia leo.

Dkt.Chuwa amesema kuwa hatua hiyo iliyobaki itakwenda kukamilika hadi tarehe 5 Septemba, 2022 na zoezi hilo litafanyika kwa njia ya simu zilizotolewa zitatumika kuwafikia ambao hawajahesabiwa.

”Sensa ya watu na makazi imebaki asilimia 0.07 kukamilisha zoezi ambapo zoezi hilo litaendelea hadi Septemba tano mwaka huu kwa kutumia namba za simu maalumu ambazo zilitolewa na zitatumika kuwafikia ambao hawajahesabiwa kwa utaratibu maalumu kupitia viongozi wa mitaa na vitongoji.”amesema Dkt.Chuwa

Dkt.Chuwa amesema kuwa, utaratibu maalum utaandaliwa wa namna ya kuzifikia kaya hizo kupitia viongozi wa mitaa na vitongoji

“Kwa upande wa sensa ya majengo hadi kufikia leo asubuhi jumla ya majengo yaliyokwisha kuhesabiwa ni 6,351,927 ambapo taarifa za umiliki, mahali yalipo na taarifa nyingine zilizoaizinishwa katika dodoso la majengo zimekusanywa,kwa makadirio ya operesheni anwani za makazi tunategemea kuhesabu majengo yapatayo milioni 12.7 nchi nzima,"amesema.

Hata hivyo, Dkt.Chuwa amesema kuwa sensa ya majengo Dodoso lake linamaswali 27, taarifa zinazokusanywa zinazohusu aina na sifa za Majengo,idadi ya majengo na Nyumba (unit)zilizopo ,hali ya ujenzi /ukaazi na sababu za jengo kutumika.

”Kama tunavyofahamu Serikali kwa Mara ya kwanza tangu tupate Uhuru mwaka 1961 sensa ya Watu na makazi ya kidigitali ambayo imejumuisha sensa ya majengo na sensa ya Anwani za makazi katika Mfumo wake wa utekekezajim,”amesema.

Dkt.Chuwa ameeleza kuwa Sensa ya Watu na Makazi hapa nchini hufanyika kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu Sura 351 kifungu kidogo cha 6(2)(a).

Aidha, amesema Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 na kama zilivyokuwa sensa nyingine zilizokwisha kufanyika hutumia miongozo ya Umoja wa Mataifa kwa kuwa matokeo yake yanatumika kitaifa na Kimataifa.

Pia amesema,bajeti ya Sensa ya Watu na Makazi inayoendelea nchi mzima iliidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka wa Fedha 2022/2023 ambapo ni kiasi cha shilingi Bilioni 400 sawa na wastani wa sh.6,265 au dola za kimarekani 2.7 kwa mtu mmoja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news