ASKOFU DKT.MWAKIPESILE: MUWE TAYARI KUHESABIWA KWA MAENDELEO YETU

NA MWANDISHI WETU

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la EAGT Dkt. Brown Abel Mwakipesile ametoa wito kwa waumini wa kanisa hilo kujitokeza kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika tarehe 23 Agosti, 2022 nchini.
Ametoa kauli hiyo wakati akihubiri kwenye ibada ya Jumapili tarehe 21 Agosti, 2022 katika kanisa lake la EAGT Mlimwa West lililopo Maili Mbili Jijini Dodoma.

Askofu Mwakipesile alisema ni jukumu la kila muumini kuwa kielelezo kizuri katika jamii kwa kuwa tayari na kuonesha ushirikiano kwa makarani wa sensa ili kufanikisha zoezi hilo.

“Kila aliyeokoka awe mfano kwenda kuhesabiwa, popote alipo mwana EAGT ahakikishe anakuwa mstari wa mbele kushiriki zoezi la sensa,”alisema Dkt. Mwakipesile.

Aliongezea kuwa, sensa ni jambo muhimu kwa kuzingatia idadi ya watu inahitajika kila eneo ikiwemo katika kanisa ili kufanishi mipango ya maendeleo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news