NA DIRAMAKINI
MMILIKI na Mkurugenzi wa Azam FC, Yusuf Bakhresa jana alikutana na wachezaji kupanga mikakati ya msimu ujao.

Bakhresa aliyekuwa na Mwenyekiti, Nassor Idrissa (Father) amefanya usajili ambao unatajwa kuwa wa aina yake kwa ajili ya kuipa mafanikio timu hiyo msimu wa 2022/2023.
Ni wachezaji ambao wanatajwa kuwa ni wenye viwango vya hali ya juu ambao huenda wakawa msaada mkubwa kwa matajiri hao ambao wamekuwa wakifanya vizuri katika soka la Tanzania.