DAVID KAFULILA: Rais Samia amevunja rekodi ya miaka 20 Sekta ya Maji, ameokoa Trilioni 3/- ambazo zingetumika kutibu magonjwa yatokanayo na maji

NA DIRAMAKINI

ALIYEKUWA Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mheshimiwa David Kafulila amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amevunja rekodi ya utekelezaji bajeti ya maji kwa miaka 20.
"Wakati nakuja Simiyu kero kubwa kuliko zote ilikuwa maji. Mwaka mmoja niliokaa hapa tumeshirikiana kusimamia mabilioni ya fedha za miradi ya maji, wote tunaona tatizo linapungua kwa kasi.

"Kutoka upatikanaji wa maji wa asilimia asilimia 56 mwaka 2020 mpaka asilimia 73 kufikia Juni 2022.

"Hii ni mbali ya mradi mkubwa wa bomba la kilomita 190 kutoka Ziwa Victoria wenye thamani ya shilingi billioni 400 utakaopita zaidi ya vijiji 200 ambao kazi za awali zimeanza...

"Hongera sana Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan. Niwaambie ukweli,nimesoma bajeti ya miradi ya maji za miaka 20 kuanzia mwaka 2000 mpaka 2020, hakuna mwaka ambao fedha za miradi ya maji zilitolewa asilimia 80.

"Bajeti ya kwanza ya Awamu ya Sita ( 2021/22) fedha za miradi ya maji billioni zilizotolewa ni billioni 743 sawa na asilimia 95 ya bajeti iliyopitishwa na Bunge zimetolewa ndani ya miezi tisa tu.

"Sio mwaka. Huu ni ushahidi kuwa Rais wetu anatekeleza kauli mbiu yake ya kumtua maam ndoo kichwani kwa vitendo. Anaelewa kuwa maji ni uchumi, maji ni ustaarabu, maji ni afya,"amefafanua Mheshimiwa David Kafulila.

Kwa mujibu wa Mheshimiwa Kafulila, Ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO) mwaka 2014 ilionesha kuwa kwenye kila dola moja inayowekezwa kwenye maji, inaokoa dola 4.2 ambazo zingetumika kutibu magonjwa yanayotokana na ukosefu wa maji safi na salama (UN-News, Nov19, 2014).

"Hivyo billioni 743 za miradi ya maji katika mwaka mmoja wa 2021/22 ni sawa na kuokoa trilioni 3.1 ambazo zingetumika kutibu magonjwa yatokanayo na maji. Labda niwakumbushe tu kwamba utafiti uliofanywa na taasisi ya SYNOVATE mwaka 2008 ulionesha kuwa kero namba moja kwa Mtazania ni maji.

"Hii ni taasisi ya tano kwa sayansi ya uratibu wa maoni duniani wakati huo kabla haijachukulia na IPSOS ambayo kwa sasa ni moja ya taasisi tatu kubwa duniani kwa kazi hiyo (OPINION SURVEY).

"Hiki ni kielelezo kuwa, Kiongozi anaetatua tatizo la maji, anagusa maisha ya watanzania walio wengi na hasa vijijini ambao inawezekana hawana kelele nyingi kwenye mitandao...wanaitwa ' silent majority'.

"Hivyo tunaposema Mama anaupiga mwingi sio sisi ni takwimu za kitafiti.Hivyo tuendelee kuwasaidia wananchi kwa kuhakikisha wakandarasi wanatekeleza mikataba na tuendelee kuvunja mikataba ya wababaishaji kama tulivyofanya siku zote kuhakikisha kuwa fedha anazoleta Mhe.Rais kukabili kero ya maji zinafanya kazi kweli kweli," amesema Kafulila leo wakati wa makabidhiano ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kati yake na Mkuu wa Mkoa mpya Dkt.Yahaya Nawanda ambapo mbali ya kueleza sura ya Mkoa wa Simiyu, Kafulila ameleza pia maamuzi tisa ya kimkakati aliyotekeleza ndani ya mwaka mmoja na mwezi mmoja wa Utumishi wake wa nafasi ya RC Mkoa huo wa Simiyu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news