NA DIRAMAKINI
MKURUGENZI wa Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya amewatoa hofu wananchi juu ya utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa vijana,wanawake na watu wenye ulemavu.

"Nikuhakikishie kuwa utoaji wa mikopo upo wazi,hakuna kikundi chochote kinachopendelewa, utaratibu unaanzia kwenye kata husika , kikundi kinatakiwa kiandae andiko na kwa kifupi ni kwamba utoaji wa mikopo hii hufuata sheria na kanuni,"amesisitiza Mabelya.

Awali akikagua baadhi ya shughuli zinazofanywa katika banda la Manispaa ya Temeke,mkurugenzi Mabelya alionesha kufurahishwa kwake mara baada ya kupata maelezo ya kina kutoka kwa wataalamu wa kilimo,mifugo na Uvuvi.