Rais Samia ampongeza Diwani wa CHADEMA Kiwira kwa mapokezi ya heshima

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amesema amevutiwa na mapokezi ya Diwani wa Kiwira, Bw. Michael Saimon kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimia wananchi wa Kiwira Wilaya Rungwe mkoani Mbeya alipokua njiani akielekea Tukuyu leo Agosti 7, 2022.

Amesema, mapokezi hayo yamevunja rekodi na Bw.Saimon amekuwa akifanya kazi kwa kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana na kusimamia vema utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

''Nimefurahishwa sana na mapokezi haya kwani haijawahi kutokea, siasa za uchaguzi zilishapita na wanapofanya kazi sio kwa wana CHADEMA peke yao bali anatekeleza ilani ya chama katika kuleta maendeleo ya Watanzania;

Mheshimiwa Rais Samia ameyasema hayo leo Agosti 7,2022 mara baada ya msafara wake kusimama na kusalimia wananchi wa Kata ya Kiwira huko Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya huku mamia ya wananchi na wafanyabishara wakijitokeza wakiongozwa na diwani huyo.

Wakati huo huo, Mheshimiwa Rais Samia amesema, kila kijana wa Kitanzania anayechaguliwa katika uchaguzi nchini anapaswa kufanya kazi za Watanzania katika kuwaletea maendeleo.

Diwani huyo, Bw.Saimon alimueleza Mheshimiwa Rais Samia kuwa, CHADEMA wanatembea kwenye njia yake kwani amewaunganisha na kitendo cha kukutana na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe kimewapa moyo na matumaini makubwa.

''Mheshimiwa Rais, tumeona namna unavyotuunganisha sisi ni watoto wako, tunaendelea kupita katika njia zako na kupokea ushauri utakaotoa kwa WANACHADEMA,"amesema Bw.Saimon.

Kwa upande wake, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt.Tulia Ackson amesema, diwani huyo licha ya kuwa CHADEMA amekuwa kiungo kwa wananchi katika kutekeleza miradi ya maendeleo inayoelekezwa na Serikali.

''Diwani wa upinzani, lakini kaweka siasa pembeni na anachapa kazi kweli kweli katika kuleta maendeleo ya wananchi wake pamoja na kueleza changamoto mbalimbali," amesema

Pia ameiomba Serikali kuona namna bora ya kutenga fedha kwa ajili ya kufanya upanuzi wa barabara kuu ya Tukuyu kwenda Kiwira ikiwa ni pamoja na kufunga taa kutokana na changamoto mbalimbali ikiwepo ajali za barabarani.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof.Makame Mbarawa amesema tayari Serikali imetenga shilingi milioni 200 kwa ajili ya kufunga taa 600 za barabarani pamoja na kuwepo kwa mikakati ya kufanya upanuzi wa barabara hiyo siku za karibuni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news