NA DIRAMAKINI
KIMISAA wa Sensa ya Watu na Makazi, Anne Makinda ameishukuru na kuipongeza Kampuni ya Doweicare Technologies kwa kutoa msaada wa taulo za kike 24,000 zikiwa na nembo ya Sensa.
Amesema taulo za kike ni sehemu ya afya ya kinamama hivyo kutolewa kwa taulo hizo wakati huu tukielekea siku ya Sensa kutasaidia kuwatia moyo wananchi kushiriki Sensa.
“Kufahamu afya za wanawake na binti zetu, kuelewa idadi yao na mahali walipo ni muhimu katika kupanga utoaji wa huduma na kupeleka maendeleo katika maeneo husika,”Mhe.Anne Makinda.
Ametoa wito kwa wananchi kujiandaa kuhesabiwa hapo tarehe 23 Agosti, 2022 na kuwataka kutoa taarifa sahihi kwani kufanya hivyo kutaihakikishia serikali kupata takwimu za idadi ya watu nchini zilizo sahihi.
Aidha, takwimu sahihi zitaisaidia serikali kupanga mipango bora yenye kuakisi hali halisi na mahitaji halisi ya wananchi wake na kufuatilia utekelezaji wa mipango hiyo.