Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof.Juma ahesabiwa na familia yake Dar es Salaam

NA MWANDISHI WETU

JAJI Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma leo tarehe 23 Agosti, 2022 ameshiriki katika zoezi maalum la Sensa ya Watu na Makazi lililoanza nchini.

Mhe. Prof. Juma ameshiriki zoezi hilo kwa kuhesabiwa na Karani wa Sensa, Bi. Yvonne Ngakongwa alipomtembelea nyumbani kwake Oysterbay barabara ya Kajificheni jijini Dar es Salaam.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis (kushoto) akihojiwa na Karani wa Sensa, Bi.Yvonne Ngakongwa alipomtembelea nyumbani kwake Oysterbay barabara ya Kajificheni leo tarehe 23 Agosti, 2022 kwa zoezi maalum la Sensa ya Watu na Makazi lililoanza leo nchini.

Hivi karibuni, Mhe. Jaji Mkuu alisema kuwa, “Kwa upande wa Mahakama, Sensa ni zoezi muhimu sana kwa sababu inatupa idadi sahihi ya watu itakayosaidia kuboresha zaidi huduma za utoaji haki kwa wananchi.”
Mwenza wa Jaji Mkuu, Bi. Marina Juma akishiriki katika zoezi la kuhesabiwa walipotembelewa na Karani wa Sensa, Bi. Yvonne Ngakongwa.(Picha na Mary Gwera, Mahakama).

Mhe. Prof. Juma alisema hivyo, na kutoa rai kwa wananchi kushiriki katika zoezi hilo muhimu kwa uboreshaji wa huduma za utoaji haki na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news