Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Philip Isdor Mpango leo Agosti 23, 2022 pamoja na mke wake,Mbonimpaye Mpango wameshiriki kwenye shughuli ya Sensa ya Watu na Makazi wakati Karani wa Sensa Isack Mgosho alipofika kwa ajili ya kuwahesabu katika makazi yao Chanika jijini Dar es Salaam.