Mapinduzi FC yatwaa ubingwa Utalii Cup

NA DIRAMAKINI

TIMU ya Mapinduzi FC imeibuka washindi katika mashindano ya Utalii Cup yaliyokuwa yakifanyika katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Mmashindano hayo yamemalizika Agositi 27,2022 ambapo mshindi wa kwanza Mapinduzi FC alipata zawadi ya shilingi milioni tano pamoja na kikombe huku mshindi wa pili Copco Fc alipata milioni tatu,mshindi wa tatu milioni moja na nusu na mshindi wa nne alipata laki tano.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo Afisa Utalii Mwandamizi, Daines Kunzugara alisema mashindano hayo yamekuwa chachu katika Mkoa wa Mwanza kwa kuhamasisha vijana kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo Kisiwa cha Sanane.

Kunzugara ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Mwanza kuwa wazalendo kwa kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo mkoani hapa.

Akizungumzia siri ya ushindi wa Mapinduzi FC kocha wa timu hiyo, Magogo Mataba,amesema kuwa, wachezaji wameonyesha uwezo wao wa kucheza kwa kutulia katika kipindi chote cha mashindano.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news