NA DIRAMAKINI
WANANCHI na mashabiki mbalimbali wa Klabu ya Yanga, wamempongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa hatua yake na kuhamasisha wananchi kushiriki zoezi la Sensa ambayo itafanyika Agosti 23, 2022.
Sensa
ya Watu na Makazi ni zoezi la kitaifa linalofanyika kila baada ya miaka
10 ambapo Sensa ya mwisho kufanyika nchini ni ile ya mwaka 2012.
Hivyo
Sensa ya mwaka 2022 itakuwa ni sensa ya sita kufanyika nchini baada ya
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964. Sensa nyingine
zilifanyika mwaka 1967, 1978, 1988, 2002 na 2012.
Umuhimu wa kipekee wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ni pamoja na:-
Kuisadia
Serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidia mchakato wa
utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025, mageuzi ya masuala ya
afya na jamii, pamoja na ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo za
kimataifa;
Taarifa
za idadi ya watu husaidia katika mamlaka za wilaya katika utekelezaji
wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi
husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimali.
Taarifa za msingi za hali ya kidemografia, kijamii na kiuchumi za idadi ya watu na makazi za mipango katika ngazi zote;
Kigawio
katika kukokotoa viashiria vingine mfano Pato la mtu mmoja mmoja, Pato
la Taifa, Ajira na ukosefu wa Ajira na kiwango cha uandikishaji wa
wanafunzi;
Taarifa
itakayowezesha serikali kujua ongezeko la idadi ya watu, kwa mgawanyo
na viashiria vingine, ambavyo ni muhimu kwa usimamizi wa mazingira; na
Msingi
wa utawala bora na ujumuishaji wa demokrasia. Takwimu sahihi za Sensa
zinahitajika kwa ajili ya ugawaji wa majimbo ya uchaguzi kwa ufanisi,
kurekebisha mipaka ya kiutawala katika serikali za mitaa.
Sensa ya 2022 inatarajiwa kuwa na vitu vipya
1:Kutenga
maeneo ya kijiografia ya kuhesabia watu katika ngazi za kitongoji/mtaa
na upatikanaji wa taarifa za kitakwimu katika ngazi za kitongoji/mtaa
pamoja na kuwa na mipaka ya kudumu katika ngazi hizo;
2:Matumizi ya Vishikwambi (tablets) katika hatua zote za utekelezaji wa sensa kwa lengo la kupunguza gharama;
3:Nyongeza ya maswali yatakayowezesha upatikanaji wa taarifa zaidi za kitakwimu ikilinganishwa na Sensa ya Mwaka 2012:-
Taarifa za kidemografia (umri wakati wa ndoa ya kwanza);
Maswali yanayohusu ulemavu (Kichwa kikubwa, Mgongo wazi, Kifafa/Epilepsy, Mbalanga/storiasis na Usonji/autism);
Maswali ya uhamaji kulingana na mapendekezo ya IOM (International Organization of Migration);
Maswali
kuhusu umiliki wa nyaraka za kitaifa (vitambulisho NIDA, vitambulisho
vya wafanyabiashara wadogo wadogo, Mzanzibari mkazi, hati ya kusafiria,
na leseni ya udereva);
Maboresho ya maswali ya shughuli za kiuchumi ikiwa ni pamoja na idadi ya kaya ziliko kwenye sekta isiyo rasmi;
Umiliki wa ardhi na taarifa za TEHAMA
Takwimu za nyumba (orodha, hali ya umiliki na aina ya nyumba)
• Maswali ya kilimo na mifugo