NA DIRAMAKINI
KIONGOZI wa Kanisa la Inuka Uangaze (Arise and Shine),Nabii na mtume Boniface Mwamposa (Bulldozer) ameweka bayana utayari wake katika zoezi la kuhesabiwa kupitia Sensa ya Watu na Makazi Agosti 23, mwaka huu.
Mwamposa ambaye amekuwa kiongozi mahiri wa imani ya Kikristo nchini hata kujizolea umaarufu mkubwa kama "Bulldozer" ameeleza namna zoezi la sensa lilikuwa likifanyika hata zamani katika vitabu vitakatifu vinajieleza na kuwaasa watanzania kutopotoshwa juu ya zoezi la kuhesabiwa nchini.
"Sensa ni jambo la baraka kiimani, wakati Yesu anazaliwa ilitangazwa amri na Kaisari kuwa watu wote wahesabiwe, hata Yesu alipozaliwa alizaliwa katika holi la ng'ombe sababu nyumba za wageni zilijaa watu waliokuwa wamerudi kwao kuhesabiwa,"amesema.
Mchungaji Mwamposa amewaasa watanzania kujitokeza kuhesabiwa na kufurahia jambo hilo kwani linaleta baraka kwa wananchi na nchi kiujumla.
"Furahia kuhesabiwa ili ujulikane kama mmoja wa watanzania walio mchini, mimi,"amesema.