Orodha ya Waombaji waliodahiliwa zaidi ya Chuo Kimoja au Programu zaidi ya moja katika awamu ya Kwanza kwa mwaka wa masomo 2022/2023

NA GODFREY NNKO

TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imesema kuwa, awamu ya kwanza ya udahili kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza katika Taasisi za Elimu ya Juu nchini kwa mwaka wa masomo 2022/2023 imekamilika.

Prof. Charles D.Kihampa ambaye ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ameyabainisha hayo leo Agosti 24, 2022 jijini Dar es Salaam ambapo majina ya waliodahiliwa katika awamu hii yanatangazwa na vyuo husika.Soma kwa kina hapa>>>

Amesema, katika Awamu ya Kwanza ya udahili, jumla ya waombaji 106,295 wametuma maombi ya kujiunga katika vyuo 76 vilivyoidhinishwa kudahili.

Aidha, jumla ya programu 757 zimeruhusiwa kudahili ikilinganishwa na programu 724 mwaka 2021/2022. Vilevile kwa upande wa nafasi, mwaka huu kuna jumla ya nafasi 172,168 ikilinganishwa na nafasi 164,901 mwaka uliopita.

"Hili ni ongezeko la nafasi 7,267 sawa na asilimia 4.4 katika programu za Shahada ya Kwanza. Pia katika Awamu ya Kwanza ya udahili, jumla ya waombaji 75,163 sawa na asilimia 70.71 ya waombaji wote walioomba udahili wameshapata udahili vyuoni.
Hii hapa orodha ya Waombaji waliodahiliwa zaidi ya Chuo Kimoja au Programu zaidi ya moja katika awamu ya Kwanza kwa mwaka wa masomo 2022/2023 BOFYA HAPA KUPAKUA MAJINA YOTE>>>

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news