NA GODFREY NNKO
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo Agosti 13, 2022 amefanya uteuzi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo Agosti 13, 2022 amefanya uteuzi.
Mosi, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amebadilisha uteuzi wa Bi.Mtumwa Khatib Ameir kutoka Mwenyekiti wa Bodi ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara katika Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango.
Aidha, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Luteni Kanali mstaafu Amour Jen Ally kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA) katika Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi.
Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said, uteuzi wa Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi unaanza leo.