Rais Dkt.Mwinyi apokea jopo la madaktari kutoka Korea Kusini

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema ujio wa madaktari kutoka Jumuiya ya ‘Korea National Turbaculosis Association’ utafungua milango kwa madaktari na wataalamu wa afya wa Taifa hilo kuja nchini kuwasaidia Wazanzibari katika kukabiliana na maradhi mbalimbali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi (kulia) akizungumza na ujumbe wa madaktari kutoka Jumuiya ya Korea National Turbaculosis Assosiation, inayoshuhulikia maradhi ya Kifua Kikuu (TB), walipofika Ikulu jijini Zanzibar leo, wa tatu kulia ni Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Dkt.Kyung Manho.(Picha na Ikulu).

Mheshimiwa Dkt.Mwinyi amesema hayo Ikulu jijini Zanzibar alipozungumza na timu ya madaktari 15 kutoka Jumuiya ya Korea National Turbaculosis Association ya nchini ya Korea Kusini, waliokuja nchini kwa ajili kambi ya uchunguzi na matibabu ya ugonjwa wa kifua kikuu (TB).

Amesema, Zanzibar inakabiliwa na magonjwa mbalimbali, ikiwemo TB na akabainisha mahitaji makubwa yaliopo katika upatikanaji wa madaktari na wataalamu wengine wa afya ili kukabiliana na magonjwa hayo.

Amesema ujio wa madaktari hao utatoa fursa kwa madaktari wazawa na wafanyakazi wa afya kushirikiana na madaktari wa timu hiyo na kujenga uwezo katika kakabiliana na ugonjwa huo, huku kukiwepo matarajio makubwa ya kuleta tija.

Aidha, ametoa shukrani kwa madaktari hao kwa dhamira ya kuja nchini kuwasaidia Wazanzibari na kusema Zanzibar inatambua hatua kubwa iliofikiwa na Taifa la Korea Kusini katika kupambana na magonjwa mbalimbali, ikiwa na madaktari na wataalamu wa afya katika nyanja mbalimbali.
Mapema, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Korea National Turbaculosis Asssociationa, Kyung Manho alisema jumuiya hiyo imefanya ziara ya kuja Zanzibar ili kujenga ushirikiano kati yake na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kukabiliana na maradhi ya TB.

Amesema, hatua hiyo ni kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya Zanzibar na Taifa hilo la Korea Kusini.

Jumuiya ya Korea National Turbaculosis inayojishughulisha na kinga na matibabu dhidi ya ugonjwa wa TB, ilianzishwa mwaka 1953, ikiwa ni mara ya kwanza kufika hapa nchini, ambapo wakiwa nchini wataweka kambi na kutoa huduma za tiba kwa wagonjwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news