
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema wakati wakisalimiana na viongozi mbalimbali waliofika kwenye mapokezi katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal one Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema wakati wakiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za asili na matarumbeta vilivyokuwa vikitoa burudani wakati wa mapokezi katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal one Jijini Dar es Salaam.