Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, akihesabiwa na Karani wa Sensa, Jasmini Kinga katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi nyumbani kwake Mtaa wa Utemini mkoani hapa leo hii Agosti 23, 2022.
Karani wa Sensa ya Watu na Makazi, James Rutihinde akijitambulisha kwa Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko kabla ya zoezi hilo lililofanyika nyumbani kwake mkoani hapa.
Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Mulagiri akihesabiwa na Karani wa Sensa, Peter Samike katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi nyumbani kwake mkoani hapa leo hii Agosti 23, 2022.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alhajj Juma Killimba akionesha furaha yake kabla ya kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi lililoanza leo.
Mratibu wa Sensa ya Watu na Makazi Mkoa wa Singida, Nying'oya Kipuyo, akitoa maelezo mafupi kabla ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba ajahesabiwa.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Alhajj Juma Killimbah akihesabiwa na Karani wa Sensa, Flora Mkumbo, katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi nyumbani kwake mkoani hapa leo hii Agosti 23, 2022.